KUWEPO KWA OFISI ZA WABUNE NDANI YA MAJIMBO KUNARAHISISHA UTENDAJI KAZI WA VIONGOZI.

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira mh. Januari yussuf makamba, amesema kuwepo kwa ofisi za wabune ndani ya majimbo kunarahisisha utendaji kazi wa viongozi hao katika kutatua kero za wananchi.

Akizungumza baada ya kukabidhi ofisi ya wabunge katika jimbo la kiwengwa iliopo kitope, kwa waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais mh. Muhammed aboud, waziri makamba amesema hatua hiyo itasaidia wabunge kufanya kazi zao katika majimbo na kuleta maendeleo kwa haraka.


Aidha mh. Makamba amezitaka taasisi za muungano zisizo na ofisi zanzibar kujenga ofisi hizo ili kutekeleza shughuli zinazohusu masuala ya muungano na kupunguza malalamiko.

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais mh. Muhammed aboud, amesema uwepo wa ofisi hiyo utasaidia utekelezaji wa mpango wa serikali wa madaraka mikoani kwa kutuyatumia kwa shughuli mbalimbali.

Baadhi ya wananchi na shehia ya kitope mbaleni wamesema ni jambo la faraja kukabidhiwa ofisi hiyo kwani itawapa fursa ya kuonana na viongozi wao kwa urahisi katika kutafutiwa ufumbuzi matatizo yao.
chanzo: zbc.

Comments