Kutoa taarifa mapema kuhusu utafiti wa mpango wa kunusuru kaya masikini kwa wananchi.

Viongozi wa shehia wameshauriwa kutoa taarifa mapema kwa wananchi wanaohusika na utafiti wa mpango wa kunusuru kaya masikini unaotarajiwa kufanyika mwazi ujao ili kurahisisha ukusanyaji wa taarifa zao.

Mratibu wa mradi wa utafiti wakutathimini kaya masikini awamu ya pili upande wa zanzibar bi asya takrima amesema mara nyingi watendaji wamekuwa wanakosa taarifa katika baadhi ya kaya kutokana na wahusika kutofikisha taarifa mapema.


Akizungumza katika majaribio ya kazi ya utafiti huo uliofanyika katika shehia ya fuoni birikani ,chunga na kibondeni amesema mara nyingi kitendo hicho kinakwamisha kupatikana taarifa muhimu za tathmini kwa kaya ziliomo katika mpango huo.

Mratibu wa mradi huo kutoka bank ya dunia tumainieli ngowi amesema utafiti huo kuanza kutumika kwa njia ya kielektoroniki umerahisisha utendaji wa kazi hiyo.

Wadadisi wanaoshirikia kazi hiyo wameelezea walivyofanikiwa katika utafiti huo wa majaribio
Utafiti huo wa mradi wa utafiti wakutathimini kaya masikini awamu ya pili unatarajiwa kuanza august 7 nchini kote litahusisha shehia 90 .
chanzo:Zbc.

Comments