Kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa.

Kamishna wa kikosi cha vyuo vya mavunzo ali abdallaAli, amewahimiza walinzi wa kikosi hicho kusimamiaUzalishaji wa mazao ya chakula kwakuzingatia kuwaKilimo ndio uti wa mgongo wa taifa.

Akizindua uvunaji wa mpunga katika bonde la langoni amesema askari katika taifa lolote wanatakiwa kuwa mstari wa mbele na kuwa tayari kwaajili ya kujenga uchumi wa nchi yake.


Amefahamisha kuwa jeshi likisimama imara katika uzalishaji wa mazao ya chakula kutasaidia kubana matumizi kwa ununuzi wa chakula kutoka nje ya jeshi hilo.

Nae asp, amour naim, akitoa tathmini juu ya uvunaji huo wa mpunga na mahindi amesema katika mavuno ya msimu huo jumla ya ekari kumi zimevunwa na kusaidia kwa matumizi ya ndani kwa kikosi hicho cha mafunzo.
chanzo:Zbc.

Comments