Kwa mujibu wa sheha wa shehia hiyo Mohammed Ameir Khamis amesema,
tukio hilo limetokea jana Julai 17, 2017 majira ya saa moja asubuhi
baada ya watoto waaliokuwa wakiokota chupa kukikuta kichanga hicho
katika jaa hilo.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamishna msaidizi
mwandamizi wa polisi Hassan Nassir Ali akithibitisha kutokea kwa tukio
hilo amesema: “maiti hiyo imetupwa jaani na mtu asiyejulikana na
ilipelekwa hospital ya Mnazi mmoja uchunguzi wa daktari umefanyika na
upelelezi wa polisi unaendelea”.
Aidha Kamanda Hassan amewataka wazazi kuacha tabia hizo zisizokuwa za kiuungwana.
chanzo:zanzibar24.
Comments