
Mh.Ally Happi alitoa amri hiyo kwa jeshi la polisi baada ya Halima mdee kutoa kauli zinazodaiwa kuwa ni za kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.
Leo jumatano ya July 5, 2017 Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo
Zitto Zubeir Kabwe ameamua kupaza sauti ya jambo hilo ambapo kupitia
ukurasa wake wa facebook ameandika Amri ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni
kumkamata Mbunge Halima James Mdee ni mwendelezo wa matumizi mabaya ya
madaraka.
Hayapa chini maneno kamili alio andiko Zitto kabwe kwenye facebook yake
Amri ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni kumkamata Mbunge Halima James Mdee ni mwendelezo wa matumizi mabaya ya madaraka. Inasikitisha Sana kuona viongozi vijana wanafanya mambo ya hovyo Kabisa. Sheria ya DC kumweka mtu kizuizini Ina masharti yake na haihusiani kabisa na yanayoitwa makosa ya ndugu Halima Mdee. Tunapaswa kulaani Kwa nguvu Sana mambo haya kwani yataota mizizi na kuathiri watu wengi zaidi.
chanzo:zanzibar24.
Comments