Jumuia ya Ismailia Agakhan yaiunga mkono SMZ.

Image result for newsJumuiya ya Ismailia  Mtandao wa Maendeleo wa Agakhan imesema  inaendelea  kuiyunga mkono  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kusaidia jamii  miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa  lengo ni  kuinua uchumi wa watu wa Zanzibar.

Akizungumza katika Sherehe ya kumbukumbu  za kuadhimisha  Miaka 60 ya Mstahahiki Karim Agakhan Mwenyekiti  wa Ismailia Agakhan Zanzibar Zulfikar Bhaloo amesema Jumuiya yao imekuwa  mstari wa mbele  kusaidia  jamii katika    nchi mbalimbali duniani  kwa kutoa huduma   za  maendeleo ikiwemo sekta ya  Afya,Elimu, na usaidizi  wa kutengeneza  mazingira  bora ya  kujitengemea   katika miradi ya maendeleo.


Hata hivyo Bhaloo amesema Jumuiya hiyo ikisaidia miradi mengi ya maendeleo nchini Zanzibar ikiwemo Miradi ya elimu salama mtoto  kwa mtoto,Mradi wa bustani ya forodhani  na Mradi wa Hoteli ya Zanzibar  Serena  ambao   unachangia  mapato  katika mfuko mkuu wa serikali  na kuwataka wananchi kuvienzi  vitu hivyo ili viwe  histori kwa zanzibar.

Mapema akifungua sherehe hizo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohammed Mahmoud amesema Mstahahiki Karim Agakhan alitoa mchango mkubwa Zanzibar ambao umeleta maendeleo  na kuinua  uchumi  wa watu wa zanziabr.

Amesema Zanzibar bado inahitaji  wawekezaji  kuwekeza Zanzibar  ili  kusaidia  kukuza na kuinua uchumi wa nchini  kwalengo la kuleta maendeleo.

Sherehe  hizo pia ziliambatana na  uzinduzi wa Nembo  ya kumbukumbu  ya miaka 60  ya Uongozi wa Shekh Karim Agakhan ambayo ilizinduliwa na mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Ayoub Mahmoud.
chanzo:zanzibar24.

Comments