Jeshi la Polisi laendeleza msako kwa wanaorejesha nyuma maendeleo Zanzibar.

Jeshi la polisi Zanzibar limesema litaendelea kupambana na vikundi vya wizi wa aina mbali mbali ikiwemo wizi wa mifugo unaorejesha nyuma maendeleo ya wananchi katika jamii.

Akizungumza na Zanzibar24 huko ofisini kwake Madema Mjini Zanzibar Kamanda wa Polisi Mkowa wa Mjini Hassan Nassir amesema kumejitokeza baadhi vya vikundi vinavyojihusisha na wizi katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar jambo linalowatia hasara kubwa wafugaji.


Amesema katika kukomesha vitendo hivyo Jeshi la polisi katika Wilaya ya Magharib A na B tayari linaendelea na hatua ya kuvitafuta vikundi hivyo ambapo kwa sasa Baadhi ya wahusika wa wizi wa mifugo wameshakamatwa.

”tumeanza kupeleleza ni nani anaefanya vitendo hivi na kuna washtakiwa wachache wamesha kamatwa pale Fuoni na kuna kazi kubwa tunafanya na karibuni wizi huu utaisha nako huko maungani tatizo hilo lipo mda mrefu na mpaka sasa washtakiwa tumesha wakamata, sasa hawa wa fuoni nao tutawakamata wananchi watulie na waendeleee kutupa taarifa”

Aidha kamanda Nassir ametowa wito kwa jamii kuendelea kuwa waangalifu juu ya mifugo yao pamoja na kuacha tabia ya kujichukulia hatua mikononi mwao pindipo watawakamata wizi hao jambo ambalo ni kinyume na taratibu zilizowekwa .

chanzo:zanzibar24.

Comments