
Hayo ameyasema huko kisiwani Pemba alipo, kuwa katika kikao kazi na
watendaji wa Jeshi la Polisi wa mikoa miwili ya Pemba yenye lengo
la kujitambulisha toka aliposhika nafasi ya kuwa Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini na kuchukua nafasi ya mtangulizi wake ambaye ni Mkuu wa
Jeshi mstaafu Ernest Mangu.
IGP Sirro amesema kuwa, katika hatua za kukabiliana na matukio ya
kihalifu ikiwamo biashara haramu ya kusambaza na kuuza dawa za kulevya
ni vyema Askari kote nchini wakatimiza wajibu wao kwa kufuata misingi
ya sheria na taratibu.
Alisema katika awamuyake ya uwongozi amedhamiria kuona kila askari
anapenda kazi na kutumia muda mwingi katika kutekeleza majukumu yao na
kuhimiza umoja upendo na mashirikiano miongoni mwao.
Alisema mgawanyo wa idara zlizomo ndani ya jeshi hilo hazifanyi
askari kujiona bora na kumdharau mwengine bali kila askari anawajibu wa
kujenga mashirikiano na mwenzake ilikuhakikisha lengo la jeshi la polisi
la ulinzi wa raia na mali zao linafikiwa.
Mapema Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi alifika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa
kusini Pemba na kujitambulisha Mbele ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na
usalama kisiwani Pemba.
Aidha aliihakikishia kamati hiyo kuwa, Jeshi la Polisi nchini
litahakikisha linaendelea kudumisha hali ya ulinzi na usalama kwa
mashirikiano makubwa na kuwapongeza kwa kuendelea kukifanya kisiwa cha
Pemba kuwa katika hali ya amani na utulivu mkubwa.
chanzo: zanzibar24.
Comments