Kamisheni ya Utalii Zanzibar imesema itawachukulia hatua za kisheria wananchi wanaofanya hujuma katika fukwe za bahari kwa
uchimbaji wa mchanga kwani kufanya hivyo ni kuondoa
haiba na kutapelekea kushusha kipato katika sekta ya utalii.
Akizungumza na Zanzibar 24 Afisa Uhusiano kamisheni ya utalii
Mohammed Nassor Bajuni amesema fukwe ni miongoni mwa vivutio vya
utalii kwa wageni wanaotembelea Zanzibar lakini cha kusikitisha baadhi
ya wananchi wanaoishi karibu na bahari huzitumia vibaya fukwe kwa
kuzifanyia uharibifu na kusababisha fukwe zile kuharibika na kupoteza
ubora wake.
Hata hivyo Bajuni amesema serikali za Wilaya na Mikoa kwa
kushirikiana na Vikosi vya SMZ bado wananafasi kubwa
ya kuzisimamia na kuzifanyia ulinzi kwa umakini mkubwa fukwe ili
kuzinusuru na uharibifu huo kwani utalii wa zanzibar unategemea fukwe
katika mapato yake.
Amesema uharibifu huo umekuja mara baada ya serikali kuzuiya
uchimbaji wa mchanga na wananchi kuhamia katika fukwe za bahari hivyo
ametoa wito kwa wananchi kuwacha tabia ya uharibifu na badala yake
kuzilinda kwani faida yake ni kubwa katika taifa na hata wao wenyewe.
Sekta ya utalii Zanzibar inavivutio vingi ambavyo huwavutia wageni
wanaotembelea Zanzibar miongoni mwao ni fukwe,majengo ya
kihistoria,mapango,mji mkongwe na misitu ya asili pamoja na wanyama
pori.
chanzo: zanzibar24.
Comments