Majaliwa: Serikali haipendezwi na vifo vya uzazi.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali haipendezwi na vifo vya uzazi na hivyo imetenga Sh 7 bilioni kwa ajili ya kununua dawa na vifaa tiba vitakavyosaidia kuzuia vifo hivyo.
Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumatano Julai 5) wakati akihitimisha mkutano wa saba wa bunge na kuwataka wahudumu wa afya kuzingatia sheria na maadili ya afya kuwalinda akinamama wanaojifungua.

“Wanaofariki wakati wakijifungua ni mama zetu, wadogo zetu, dada zetu na wanetu, haipendezi kuona wanakufa na ndiyo maana Serikali imetenga kiasi hicho cha fedha Sh7bilioni kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wanaojifungua,” amesema.
Waziri Mkuu amesema fedha hizo zitatumika kununua dawa za kuzuia damu kutoka, dawa za kuongeza damu na  kuhakikisha hakuna mama anayefariki kwa sababu ya
 chanzo:Mwananchi.

Comments