Tume ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kwa kushirikiana na
kikosi maalumu cha jeshi la polisi wamekamata na kuteketeza magunia
zaidi ya 400 ya bangi katika kijiji cha Engalaoni wilayani Arumeru
mkoani Arusha.
Kamishna wa Intelijensia wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na
dawa za kulevya nchini, Bw Fred Kibuta amesema magunia hayo yalikuwa
yamefichwa kwenye nyumba katika kijiji hicho ambacho wakazi wake
wametelekeza nyumba zao na kukimbilia porini kukwepa kukamatwa.
Naye Kamishna wa Oparesheni ya kudhibiti dawa za kulevya nchini,
Mihayo Msikela amesema baadhi ya viongozi wa eneo hilo wanahusika katika
ulimaji na uuzaji wa bangi, jambo ambalo linahitaji ushirikiano mkubwa
toka kwa wananchi ili kudhibiti.

chanzo: zanzibar24.
Comments