
Mwanamke huyo anaejulikana kwa jina la Bi. Nuru Saleh Mzee mwenye
miaka 54 mkaazi wa Kwaalinatu mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, amekamatwa
na kete 108 za unga unaoaminika kuwa ni dawa za kulevya wakati alipokuwa katika harakati za usambazaji wa dawa hizo kwa Vijana.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha kupambana na dawa za kulevya
Mrakibu wa Polisi Omar Khamiss amesema jeshi la polisi limejipanga
vikali kupambana na watumiaji na wasambazaji wa dawa za kulevya na teari
kuna kesi nyingi wameshazifikisha mahakamani.
“kuna kundi kubwa la vijana wanasema teari wamejirudisha
katika hali ya kawaida lakini bado naamini kwamba ili wabaki salama basi
dawa za kulevya ziwe hazipo nchini” alisema polisi huyo.
Hivyo mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu zitakapo kamilika.
chanzo: zanzibar24.
Comments