Kamati
Kuu ya CHADEMA imekutana kwa siku mbili, tarehe 29 hadi 30 Julai,
2017 katika Hotel ya Double Tree, jijini Dar es Salaam kujadili hali ya
siasa nchini pamoja na ukandamizwaji wa demokrasia .
Taarifa
iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya
Nje, John Mrema inasema kwamba katika mambo ambayo Kamati Kuu imejadili
ni pamoja na kamata kamata inayoendelea kufanywa na vyombo vya dola
dhidi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA maeneo mbalimbali
nchi nzima.
Hata
hivyo kikao hicho kilijadili na kufikia maadhimio na hatua za kuchukua
katika ajenda ambapo ni pamoja na kuporomoka kwa uchumi na hali ngumu
ya maisha kwa watanzania, ambapo taarifa kamili juu ya maadhimio hayo
na hatua zitakazochukuliwa na chama itatolewa leo Jumatatu tarehe 31
Julai 2017, kwenye kikao na waandishi wa habari kitakachofanyika jijini
Dar es salaam.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments