Mbunge
wa Singida Mashariki (CHADEMA) na Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania,
Mhe. Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana ya Milioni 10 leo katika kesi
yake iliyokuwa inamkabili ya uchochezi.
Mahakama
ya Kisutu imempa dhamana Mh Tundu Lissu kwa sharti la kuwa na wadhamini
wawili watakaosaini dhamana ya thamani ya milioni kumi.
Aidha,
Mahakama hiyo pia imemtaka Tundu Lissu kutokuondoka nje ya jiji la Dar
es Salaam bila kuwa na kibali maalum cha mahakama. Uamuzi huo umetolewa
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam,
Wilbard Mashauri.
Upande
wake Tundu Lissu alikuwa anatetewa na jopo la mawakali 18 likiongozwa
na Fatma Karume na Peter Kibatala ambapo katika shauri la kwanza
waliomba Mahakama impe dhamana mteja wao.
Tundu
Lissu alitiwa katika mikono ya dola mnamo Julai 20 siku ya Alhamsi
katika uwanja wa ndege akiwa anaelekea nchini Rwanda. na siku
iliyofuata jeshi hilo lilikwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa Mbunge
huyo.
Aidha kesi yake imepangwa kusikilizwa Agosti 24 mwaka huu baada ya wadhamini wake kukamilisha taratibu zote za kumdhamini.
==>Ulizisoma hizi??
1. Nafasi za kazi: Program Manager Anahitajika
2.Nafas za Kazi: Commercial Director Anahitajika
3.Vacancy: Assistant Project Manager
==>Ulizisoma hizi??
1. Nafasi za kazi: Program Manager Anahitajika
2.Nafas za Kazi: Commercial Director Anahitajika
3.Vacancy: Assistant Project Manager
chanzo:Mpekuziblog.
Comments