Mkuu wa wilaya ya mjini marina joel thomas amesema uwepo
wa gereji hiyo kunasababisha hata uchafunzi wa kianzio cha maji na
mtaro uliopo eneo la skuli.
Naibu mkurugenzi baraza la manispaa ya mjini ali abdalla
natepe amesema baraza limepanga kulitumia eneo hilo kwa shughuli
nyengine ili kuepusha athari.
Mwalimu mkuu wa skuli ya lumumba mussa hassan ameelezea
kutoridhishwa na hali iliyopo katika eneo hilo kutokana na kuwatia hofu
huku vijana wanaofanyakazi katika gereji hiyo wakiomba kupatiwa
mazingira bora ya kuendeleza shughuli zao za kujipatia kipato.
chanzo:Zbc.
Comments