
Alisema hatua hiyo itaendeleza ushirikiano wa Uhusiano wa muda mrefu
uliopo baina ya Nchi za Miji hiyo inayofanana Kisiasa na Kimazingira
kutokana ya Ujerumani Magharibi na Mashariki Kuungana pamoja na kuwa
Taifa Moja Shirikisho kama zilivyo kwa Tanganyika na Zanzibar
ziliyounda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa ushauri huo wakati akizungumza na Ujumbe
wa Viongozi wa Manispaa ya Potsdam iliyopo Mkoa wa Brandenburg Nchini
Shirikisho la Ujerumani ukiongozwa na Meya wa Mji huo Bwana Jann Jackobs
aliokutana nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Alisema faida ya ushirikiano baina ya Miji ya Zanzibar na Potsdam kwa
kipindi kirefu imeanza kuleta matumaini hasa ikizingatiwa ile miradi
iliyoanzishwa kwa pamoja baina ya pande hizo mbili ya Nyumba za
Maendeleo za Kikwajuni { Majumba ya Mjerumani } pamoja na
uimarishaji wa Miundombinu ya Ujenzi wa Mitaro ya Maji Machafu katika
Manispaa ya Zanzibar.
Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande
wake itazingatia na kuona namna gani inaweza kusaidia nguvu katika
uratibu wa uendelezaji wa ushirikiano wa utendaji wa kila siku wa
Miradi ya pamoja itakayoanzishwa na Miji hiyo miwili.
Amehimiza umuhimu wa kuendeleaza mabadilishano ya ziara za mara kwa
mara kati ya Viongozi, Watendaji na hata Wananchi wa kawaida wa Miji
hiyo ikilenga kudumisha ushirikiano wa Kihistoria uliopo baina ya
Ujerumani na Tanzania na Zanzibar kwa ujumla.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuomba Uongozi huo wa Manispaa
ya Potsdam unaoongozwa na Bwana Jann Jackobs kuwa Mabalozi wazuri wa
kuitangaza Zanzibar Kiuwekezaji Nchini Shirikisho la Ujerumani.
Alisema Zanzibar hivi sasa iko mbioni kuendelea kuimarisha
miundombinu katika sekta ya Utalii inayotegemewa kuwa muhimili mkuu wa
Uchumi wa Taifa fursa ambayo wawekezaji wa Ujerumani wanaweza kuitumia
katika kuweka vitega uchumi vyao katika sekta hiyo.
Balozi Seif alisema Zanzibar kwa muda mrefu imekuwa ikitegemea Zao la
Karafuu ambalo limepitia katika mitihani mbali mbali katika vipindi
tofauti kiasi kwamba mabadiliko ya soko la Dunia limeiwezesha Zanzibar
wakati mwengine kusua sua katika ushumi wake.
Mapema Meya wa Manispaa ya Potsdam Bwana Jann Jackobs alisema mambo
ya msingi ya ushirikiano kati ya Mji wa Potsdam na ule wa Zanzibar
yameshakubalika na tayari yanawekwa saini kipindi hichi kwa ajili ya
utekelezaji wa pamoja.

Hata hivyo Meya wa Manispaa hiyo ya Potsdan alifafanua wazi kwamba
masuala ya mazingira na fursa za ajira hasa kwa Vijana yanakusudiwa
kufanyiwa utaratibu wa utekelezaji wake katika kipindi kifupi kijacho
ili kuja kusaidia kustawisha maisha ya Vijana wengi.
Manispaa ya Potsdam iliyomo ndani ya Mkoa wa Brandenburg Kilomita 15
Kusini Magharibi mwa Mji wa Berlin Nchini Shirikisho la Ujerumani ina
wakaazi wapatao Laki 167,745 kwa mujibu wa sensa ya Watu ya Mwaka 2015
ikilinganishwa na Manispaa ya Mji wa Zanzibar yenye wakaazi Laki 223,000
kwa mujibu wa sensa ya Watu na Makaazi ya Mwaka 2012.
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
chanzo: zanzibar24.
Comments