
Alisema utaratibu huo unazingatia uhusiano wa muda mrefu wa Kibalozi
uliopo kati ya Misri na Tanzania na Zanzibar kwa ujumla ambao ulianza
tokea kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika Mwaka 1961 na ule wa Mapinduzi
ya Zanzibar wa Mwaka 1964.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar
wakati akibadilishana mawazo ya Timu ya Madaktari kutoka Hospitali ya
Chuo Kikuu cha El –Shady kiliopo Alexandria Nchini Misri waliopo
Zanzibar kutoa huduma za upasuaji kwa wagonjwa mbali mbali.
Alisema alisema wakati umefika kwa Uongozi wa Vyuo Vikuu tofauti vya
Nchini Misri kuzingatia uongezaji wa fursa za masomo ya juu kwa
Wanafunzi wa Tanzania hasa katika sekta ya Afya na Elimu.
Balozi Seif alieleza kwamba hatua hiyo itasaidia kwenda sambamba na
uimarishaji wa Sera za Afya na Elimu zilizolenga kuimarisha elimu ya
Msingi kwa Wanafunzi pamoja na huduma ya afya ya Msingi hasa Vijijini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliueleza Ujumbe huo wa Madaktari
Tisa wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha El – Shady Alexandria Nchini Misri
kwamba Zanzibar imeweka mkakati wa kuwa na huduma za Afya ya Msingi kila
baada ya Kilomita Tano.
Mapema Kiongozi wa Timu ya Madaktari hao kutoka Hospitali ya Chuo
Kikuu cha El – Shady Alexandria Nchini Misri Profesa Saber Waheeb
alisema Timu yake tayari imeshatoa huduma za Afya kwa tariban Mara ya
Nnne sasa.
Profesa Waheeb alisema Wataalamu wa Timu hiyo hutoa huduma za
upasuaji kwa Watoto walioziba njia ya Mkojo, haja kubwa pamoja na uvimbe
wa Tumbo wakitarajia kuwafanyia huduma za Upasuaji wagonjwa wasiopungua
38.
Timu hiyo ya Madaktari Mabingwa wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha El
–Shady kiliopo Alexandria Nchini Misri wanamalizia kutoka huduma hizo
katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
Akiiongoza timu hiyo ya Madaktari Mabingwa wa Hospitali ya Chuo
Kikuu cha El –Shady kiliopo Alexandria Naibu Waziri wa Afya Mheshimiwa
Harous Said Suleiman alisema ujio wa Madaktari hao umeleta faraja kwa
wagonjwa mbali mbali ambao wangelazimika kutumia gharama kubwa kupata
huduma hizo nje ya Nchi.
Naibu Waziri Harous aliushukuru Uongozi wa Chuo cha El –Shady
Alexandria Nchini Misri kupitia Hospitali yake kwa uamuzi wake wa
kutenga Wataalamu wa Afya kutoa huduma Zanzibar katika mpango endelevu
unaofanyika kila kipindi.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
chanzo: zanzibar24.
Comments