
Alisema agizo hilo lazima lifanywe ndani ya muda wa Mwezi Mmoja
kuanzia sasa na ripoti kamili ya utekelezaji wake akabidhiwe katika
kipindi hicho ili kutoa fursa kwa wananchi wa maeneo hayo kuelewa
mipaka halisi ya eneo hilo na yale waliyopimiwa wao kwa ajili ya
shughuli za Maendeleo na Miradi ya Kijamii.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo wakati akizungumza na Viongozi
wa ngazi mbali mbali katika Wilaya ya Magharibi “B” baada ya kumaliza
ziara ya kutwa moja katika Jimbo la Dimani kukagua harakati za
Maendeleo pamoja na kupokea kero tofauti zinazowakabili Wananchi wa
Jimbo hilo hapo katika Skuli ya Kombeni.
Alisema mabadiliko makubwa ya uwekezaji Vitega Uchumi unaoendelea
kuimarika kwa kasi katika kipindi hichi ndani ya ukanda huo wa Kiuchumi
unatoa ishara kwa Wananchi kutambua thamani ya Ardhi kiasi kwamba
pasipo na utaratibu mzuri wa mipaka sehemu hiyo inaweza kuja kukumbwa na
migogoro ya ardhi inayoweza kuepukwa mapema.
Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haipendelei
kuona kwamba migogoro ya ardhi katika maeneo mbali mbali Nchini inazidi
kuongezeka jambo ambalo linaweza kurejesha nyuma Maendeleo
yanayokusudiwa kutandikwa kupitia rasilmali hiyo muhimu kwa Taifa na
Wananchi kwa Ujumla.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza katika kuitafutia
ufumbuzi changamoto inayotokana na matumizi ya Ardhi ni vyema kwa
Taasisi zinazohusika na usimamizi wa miradi ya Miundombinu na Uwekezaji
zikazingatia kipaumbele cha kulipa fidia wananchi ambao maeneo yao
kuchukuliwa kwa ajili ya kuendelezwa miradi na shughuli za Jamii .
Balozi Seif alisema kabla ya kuanza kwa ujenzi wa Mradi wowote wa
Uwekezaji katika sehemu yoyote ile ya Visiwa vya Zanzibar ni lazima
suala la fidia lizingatiwe kwanza ili kuepuka malalamiko ya Wananchi
wanaohusika na fidia za Mali na Vipando vyao.
Aliwanasihi Wananchi kuendelea kubeba dhima ya kushirikiana na
Wawekezaji wanaoamuwa kuweka vitega uchumi katika maeneo yao ili ile nia
thabiti inayokusudiwa na Serikali Kuu ya kukaribisha uwekezaji iweze
kufanikiwa vyema.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Viongozi pamoja na
Wananchi wa Majimbo ya Dimani na fuoni kwa uamuzi wao wa kuushirikiana
katika Miradi ya Kiuchumi na ile ya Ustawi wa Jamii na kupelekea
kupiga hatua kubwa katika maendeleo ya Kiuchumi na Ustawi wa Jamii.
Mapema Wananchi na Viongozi wa Shehia Nane zilizounda Jimbo la Dimani
walisema Huduma za maji safi na salama, ukosefu wa miundombinu imara ya
Bara bara, uchakavu wa baadhi ya majengo ya Skuli na Vituo vya Afya
ndio mambo ya msingi yenye kuleta changamoto Jimboni humo.
Walisema licha ya juhudi kubwa inayochukuliwa na Serikali kuu ya
kutoa fedha kwa ajili ya uimarishaji Miundombinu ya maji lakini bado
tatizo hilo limekuwa sugu na kuleta usumbufu na wakaishauri Serikali
kufanya uchunguzi wa kina wa matumizi ya fedha ilizotoa kwa ajili ya
kuendelezwa mradi wa Maji.
Hata hivyo Wananchi hao walisema licha ya juhudi kubwa zinazofanywa
na Viongozi wao wa jimbo katika kuwaletea maendeleo pia wameiomba
Serikali ifanye uchunguzi wa kina kuwabaini watu waliopewa maeneo kwa
ajili ya Uwekezaji na wakashindwa kuyaendeleza wanyang’anywe mara moja
na kupewa watu watakaokuwa na uwezo wa kuyaendeleza kwa faida ya Jamii.
Akitoa ufafanuzi wa baadhi ya kero zilizowasilishwa na Wananchi wa
Jimbo la Dimani kwenye Mkutano huo wa Majumuisho Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud alishauri ni vyema changamoto zote
zinazoibuka katika shehia za Jimbo hilo zikawasilishwa kwanza katika
Uongozi wa Wilaya kwa hatua ya awali.
Mh. Ayoub alisema baadhi ya changamoto inawezekana kutatuliwa ndani
ya ngazi za Majimbo, Wilaya na Mkoa badala ya mzigo huo kuwasilishwa
moja kwa moja Serikali Kuu ambayo ina majukumu makubwa ya Kitaifa
yanayohitaji kushughulikiwa.
Aliwahimiza Wananchi kuendelea kushindana katika kujiletea Maendeleo
yao huku wakielewa kwamba Serikali Kuu pamoja na viongozi wa ngazi
tofauti watahamasika kuunga mkono jitihada watakazoonyesha Wananchi
hao.
Akigusia kero zinazowasumbuwa Wananchi za upandishwaji holela wa
nauli kwa Gari za Abiria usiozingatia utaratibu uliowekwa Mkuu huyo wa
Mkoa wa Mjini Magharibi alitahadharisha wazu kwamba Uongozi wake utakaa
pamoja na Idara ya Leseni kwa lengo la kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.
Alisema tabia ya baadhi ya makonda wa Gari za Abiria kupandisha nauli
kiholela kwa tamaa ya kuata faida ya haraka inaleta usumbufu kwa
Wananchi wenye kipato cha chini na kamwe Serikali ya Mkoa wa Mjini
Magharibi haitolivumilia kero hilo kuona linaendelea.
Balozi Seif aliyeambatana na baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na Watendaji Wakuu wa Serikali alikagua Jengo
jipya la Skuli ya Fuoni linalojengwa kwa nguvu za Wananchi wenyewe
ambapo aliahidi kugharamia umaliziaji wake ili kuondoa usumbufu wa
msongamano wa wanafunzi uliofurika ndani ya Skuli hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia akaahidi kusaidia nguvu za
Wavuvi wa pwani ya Kichangani katika ukamilishaji wa Jengo lao jipya la
Soko katika Kijiji hicho lililotoa ajira za wavuvi wapatao 80 pamoja na
kuona pango la Maji safi na Salama lililopunguza kasi ya usambazaji wa
huduma za maji katika sehemu kubwa ya Jimbo la Dimani.
Baadae Balozi Seif akapata wasaa wa kukikagua kiwanda cha uzalishaji
wa Maziwa katika eneo huru la Uchumi Fumba kilichojengwa na Muwekezaji
Mzalendo na kutoa ajira kubwa kwa vijana walio wengi.
Ukaguzi huo ulikwenda sambamba na kuangalia ujenzi wa Nyumba za
Kisasa za Makaazi katika eneo la Mwambao wa Pwani ya fumba zinazojengwa
na Wawekezaji Wazalendo pamoja na wale wa Kigeni walioamua kuitumia
fursa hiyo iliyopo Zanzibar.
Balozi Seif ambae halkadhalika aliitembelea Skuli Mpya ya Sekondari
inayojengwa na Muwekezaji Mzalendo katika Kijiji cha Bwefum alielezea
faraja yake kutokana na mabadiliko makubwa ya uwekezaji yanayoendelea
kuchanja mbuga ndani ya Ukanda wa Maeneo huru ya Kiuchumi Fumba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwashukuru Wananchi wa Vijiji
vya Bweleo, Bwefum na Fumba kwa ukarimu wao wa kukubali kuwakaribisha
Wawekezaji hasa katika Sekta ya Elimu na kinachoonekana sasa kwa
Wawekezaji hao katika kuunga mkono miradi ya Jamii ni matunda ya
Uwekezaji huo.
Balozi Seif alisema Uwekezaji huo wa miradi mbali mbali ya Kiuchumi
umewezesha kuibadilisha mandhari nzima ya sehemu hiyo na kuiona ya
kuengeza kiasi kwamba ile dhamira halisi ya Serikali iliyokuwa nayo
tokea miaka ya 90 ya kulifanya eneo hilo kuwa la Mji wa Kisasa imeanza
kujichomoza pole pole.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
![]() |
Picha: Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifanya mzaha na Wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Fuoni Jimbo la Dimani baada ya kulikagua Jengo jipya la Skuli hiyo litakalosaidia kupunguza idadi kubwa ya Wanafunzi madarasani. |
![]() |
Picha: Balozi Seif na Baadhi ya Mawaziri na Watendaji Wakuu wa Serikali wakikagua shughuli za uwezekaji wa Jengo jipya la Skuli ya Msingi Fuoni linalojengwa kwa nguvu za Wananchi ambapo aliahidi kukamilisha ujenzi wake. |
![]() |
Picha: Balozi Seif Kati kati akiwa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayopub Mohamed Mahmoud Kushoto yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed wakikagua ujenzi wa Nyumba za Makaazi katika Mradi wa Baghresa Group Fumba. |
![]() |
Picha: Balozi Seif akibadilishana mawazo na Uongozi wa Timu ya CPS Live Bwana Johan Vanden Abeele na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bibi Katrin Dietzold wanaoendesha Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makaazi katika ukanda wa Maeneo huru ya Uwekezaji Fumba Wilaya ya Magharibi “B”. |

Picha: Pango la Maji safi na salama linalotoa Huduma za Maji na
salama na kusambazwa katika Vijiji vilivyomo ndani ya Jimbo la Dimani.
![]() |
Picha:Mhandisi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar {ZAWA} Nd. Hussein Hassan
Njuma wa kwanza kutoka kulia akimuelezea Balozi Seif aliyepo Kulia
yake tatizo linalolikumba pango hilo la kupunguza kiwango cha idadi ya
Lita zinazosambazwa kwa Wananchi kutokana na maji yake kuchanganyika na
Chumvi baadhi ya wakati. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Ardhi, Maji Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud. |
![]() |
Picha: Balozi Seif na Ujumbe wake akimaliza kulikagua Jengo Jipya la Soko la Samaki lililojengwa kwa nguvu za Wavuvi wenyewe wa Pwani ya Kichangani. |
![]() |
Picha: Haiba nzuri inayoonekana ya Jengo Jipya la Skuli ya Bwefum Jimboni Dimani linalojengwa na Muwekezaji Mzalendo ambalo kukamilika kwake litatoa huduma za kitaaluma kwa Wanafunzi wa Wilaya Nzima ya Magharibi “B”. |
![]() |
Picha: Meneja Mkuu wa Kiwanda cha uzalishaji wa maziwa Maeneo huru ya Uwekezaji Fumba Bwana Adson Fagundes Kulia akimtembeza Balozi Seif na Ujumbe wake ndani ya Kiwanda hicho kujionea uzalishaji wa Bidhaa hiyo muhimu kwa afya za Wanaadamu. |
![]() |
Picha: Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Viongozi wa Shehia zilizomo ndni ya Jimbo la Dimani katika Mkutano wake wa majumuisho ya ziara yake Jimboni humo hapo Skuli ya Kombeni. |
chanzo:zanzibar24.
Comments