
Mkuu wa Mkoa wa
Kaskazini Pemba Mhe Omar Khamis Othman amesema kuwa majungu na
fitna ni sumu kwa sehemu za kazi na kuwasisitiza askari hao kujengeana
heshima miongoni mwao.
Katika hotuba yake ya
Kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Vyuo vya Mafunzo Pemba,
Haji Hamoud Haji
iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Abied Juma Ali kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa amesema ili kuleta ufanisi wa kazi ni budi askari kufuata
maadili ya kazi yao .
Amesema kuwa iko haja
kwa Askari wa Vyuo Vya Mafunzo kufufua utamaduni wa kufanya kazi kwa
kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya Nchi na kuacha kufanya kazi kwa
mazoea na ubabaishaji .
Kwa upande wake Naibu
Kamishna wa Vyuo vya Mafunzo Zanzibar Haji Hamoud Haji ameahidi
kuendelea kushirikiana na askari wa Vyuo vya Mafunzo Kisiwani Pemba na
atafanya kazi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wote .
chanzo: zanzibar24.
Comments