
Polisi nchini India wanasema wamemkamata Ashok Kumar mwenye umri wa miaka 60 ambaye anatuhumiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi.
Ashok Kumar alifika nyumbani akiwa amelewa chakari Jumamosi usiku na
akaanza ugomvi na mkewe, Rupesh Singh, afisa wa ngazi ya juu wa polisi
katika mji wa Ghaziabad karibu na Delhi ameambia BBC.
Sunaina, 55, alikimbizwa hospitalini akiwa na jeraha la risasi kichwani, lakini alifariki njiani.
Bw Kumar amekiri mauaji hayo na kusema sasa anajutia kitendo chake, Bw Singh amesema.
“Mwanamume huyo [Kumar] amekuwa akinywa pombe kila siku. Mnamo
Jumamosi, alifika nyumbani amelewa na akaanza ugomvi na mkewe. Mkewe
alikuwa amekerwa na tabia yake ya ulevi na alitaka wazungumze, lakini
naye alitaka chakula mara moja,” Singh anasema.
“Alighadhabishwa na kucheleweshwa kwa chakula na akampiga risasi,” ameongeza afisa huyo.
chanzo: zanzibar24.
Comments