Amuua mkewe kwa kumchoma kisu.

Bahati Malima afikishwa Mahakamani kwa kumuua mkewe Janet Sajilo (35) kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali sehemu ya kifuani na kufariki dunia papo hapo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema  mauaji hayo yalifanyika juzi saa sita eneo la Kijiji cha Chingholwe, Kata ya Chanjale, Tarafa ya Nongwe.
 
Kamanda Matei alisema chanzo cha tukio hilo ilidaiwa ni wivu wa mapenzi na hata hivyo alisema chanzo halisi kilichosababisha mume huyo kuchukua uamuzi wa kumchoma mkewe na kitu chenye ncha kali kifuani, hakijafahamika na uchunguzi zaidi unaendelea na hatua za kumfikisha mtuhumiwa mahakamani zitafuatwa.
 
chanzo: zanzibar24.

Comments