Chama
cha ACT-Wazalendo kimemtaka Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba
kujiuzulu kwa kushindwa kuwapelekea wakulima wa korosho pembejeo kama
alivyoahidi.
Akizungumza
na Waandishi wa habari, jana Julai 30, 2017 jijini Dar es Salaam,
Katibu wa Itikadi na Uenezi ACT, Ado Shaibu alisema Serikali iliahidi
kuwapa wakulima wa korosho dawa ya kuua wadudu sulpher bure ili waongeze
uzalishaji, hivyo chama hicho kinaitaka serikali kutimiza wajibu wake
kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo na kama haiwezi kufanya hivyo
itangaze taarifa halisi za upatikanaji wa pembejeo hizo kwa wakulima.
”Sisi
kama chama cha siasa kwa kuzingatia falsafa ya chama chetu cha siasa ni
maendeleo tunaendelea kusisitiza kuwa serikali ni lazima itimize wajibu
wake wa kulinda maisha na hali za wananchi kwa kuhakikisha hakuna uhaba
wa pembejeo kwa wakulima hawa wa korosho nchini, kuhakikisha kuwa
pembejeo husika zinapatikana kwa bei ambayo watanzania wanaimudu na
zinapatikana kwa wakati.
"Ni muhimu tukumbuke kuwa unapohujumu zao la korosho unawahujumu wakulima zaidi ya 50,000 wanaojishughulisha na kilimo hicho,” alisema na kuongeza.
“Serikali
itoe taarifa za uhakika mapema kuhsu upatikanaji wa pembejeo badala ya
kutoa taarifa za hadaa. Ni bora ieleze wazi juu ya uwezo wake ili
wakulima waweze kujiandaa mapema kwa kujiwekea akiba kwa ajili ya
kununua pembejeo.
"Iwapo
serikali itakuwa haina uwezo wa kugawa salfa yote bure kama
inavyoonekana ieleze kwa undani kiwango inachoweza kutoa bure na
iimarishe mfumo wa pembejeo.”
Pia
ameitaka serikali ichukue hatua kali dhidi ya wafanyabiashara wa
pembejeo wanaopandisha bei kila siku bila kuangalia maslahi ya wakulima.
“Serikali
ifanye uchambuzi wa kina wa mahitaji halisi ya kila mkulima na kuwa na
uhakika wa bajeti yake ndipo itangaze kutekeleza mfumo wa salfa ya bure
isikurupuke kwa lengo la kutaka sifa
"Seriklai
ifanye haraka kutimiza ahadi yake ya kufikisha pembejeo ya bure kwa
wakulima wa korosho kwa kuhakikisha pembejeo ya bure kwa wakulima wa
korosho kwa kufikisha kiwango kinacholingana na mahitaji yaliyoko,” amesema.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments