
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Duniani Dkt
Tim Schilling ameeleza kuwa katika baadhi ya maeneo ya uzalishaji wa
kahawa, viwango vya joto vimeongezeka kiasi kwamba tayari viwango vya
ubora wa kahawa vimeanza kuathirika.
”Uzalishaji wa kahawa bora duniani bila shaka unakabiliwa na
changamoto tele kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, magonjwa na
wadudu, mahitaji mengine ya mashamba, upungufu wa wafanyikazi bila
kusahau kuimarika kwa idadi ya wanywaji wa kahawa duniani kila mwaka”,anaongeza Dkt Schilling.
Kupanda kwa kiwango cha joto kwa nyuzijoto 3C kumesababisha
kuongezeka kwa kiwango cha mvua kwa 15% haswa katika maeneo yanayokuzwa
kahawa kwa kiwango cha juu mno ya Minas Gerais na Sao Paolo. Hali hii
inaweza kusababisha kupungua kwa eneo zima linalokuzwa kahawa kutoka kwa
70-75% hadi 20-25%.
Ikiwa uzalishaji wa kahawa Ethiopia, kitovu cha kahawa ya hali ya juu
ya Arabica, na pia taifa linaloongoza kwa uuzaji nje wa kahawa Afrika,
huenda ukawa hatarini sana katika karne ijayo, hatua zisipochukuliwa.
“Nchini Ethiopia na kwa kweli kote duniani, hatua
zisipochukuliwa kahawa itapungua, na kuna uwezekano mkubwa ladha yake
pia itakuwa mbaya na kugharimu zaidi,” Dkt Aaron Davis, mtafiti wa kahawa katika Kew na mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo.
Wakulima maeneo ya mashariki ya nchi hiyo, ambapo mabadiliko ya tabia
nchi tayari yanaathiri uzalishaji, wametatizika miaka ya karibuni, na
wengi kwa sasa wanasema mavuno yameshuka kutokana na ukame wa muda
mrefu.
Jamal Kassim, Mkulima wa kahawa Ethiopia, ameshuhudia upungufu mkubwa wa mazao yake tangu aipande miaka kumi iliyopita.
Miti yangu ilizaa matunda mengi sana katika miaka ya kwanza lakini
sasa haizai tena. Nashindwa kukidhi mahitaji ya jamii yangu,” anasema.
Unywaji wa kahawa unatarajiwa kuzidi uzalishaji kwa mwaka wa tatu
mtawalia, kwa mujibu wa takwimu kutoka kwa Shirikisho la Kimataifa la
Kahawa (ICO).
Kwa sasa, ni shehena ya kahawa iliyohifadhiwa kutoka kwa
miaka ya nyuma ya uzalishaji kwa wingi ambayo imezuia kutokea kwa uhaba
wa kahawa au kupanda kwa bei.
chanzo:zanzibar24.
Comments