
Baadhi ya wakulima hao wamesema awali walikuwa na matumaini ya kuvuna
lakini baada ya kuingia maji chumvi imesababisha kilimo hicho kuungua.
Akizungumza na wakulima hao Naibu waziri wa nchi ofisi ya makamo wa
pili wa rais Mh Mihayo Juma Mhnunga amesema Serikali tayari wameshaiona
athari hiyo na hivi sasa wanatafuta njia ya kuliboresha tuta hilo ili
wakulima wasiathirike zaidi.
Ameshauri kuwekwa mlango wa dharura wa kusaidia kutoa maji hayo
katika mashamba na kurejesha udongo uliochukuliwa na maji ili wale
waliokuwa hawajafikwa na maafa hayo wapate fursa ya kuvuna mpunga wao.
Wakati huo huo Mh Mihayo ametembelea barabara ya Gando eneo la
Mangwena lililokatika wa mvua na kuwapongeza wafanyakazi kwa kurejesha
huduma ya usafiri kwa haraka licha ya uhaba wa vifaa walivyonavyo.
Aidha Naibu waziri huyo ameshuhudia ugawaji wa misaada ya chakula na
nguo kwa wananchi waliopatwa na maafa katika majimbo ya Kojani na
Micheweni na kuwataka kuwa na umoja na mashirikiano pale wanapokutwa na
maafa .
chanzo:zanzibar24.
Comments