Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania TIRA imesema kumekuwa na udanganyifu na ongezeko la bima bandia nchini kunakosababisha kupotea kwa mapato ya serikali hivyo mamlaka imezindua mfumo wa Tehama utakaoweza kusaidia kugundua na kuondoa bima bandia zisizo na vigezo ili kuepusha upotevu huo.
Akizungumza katika Mkutano na Askari wa usalama barabarani Mkurugenzi wa Maendeleo ya Masoko na Utafiti wa mamlaka hiyo Adelaida Muganyizi amesema kuna wimbi kubwa la udanganyifu wa bima kwa madereva wa daladala na gari za binafsi kughushi stika za bima na kusababisha hasara kubwa kwa serikali hivyo mfumo huo wa Tehama utawasaidia Maaskari wa usalama barabarani katika utekelezaji wa majukumu ya kazi yao kuweza kuwabaini madereva waliofanya udanganyifu na kuwafikisha katika vyombo vya kisheria.
Kwaupande wake Naibu Kamishina wa Usalama barabarani Mkadam Khamis Mkadam ametoa wito kwa Jeshi la Polisi hasa usalama barabarani kufanya kazi kwa mujibu wa sheria pindipo watakapo mkamata dereva na bima bandia au kughushi bima kumfikisha katika vyombo vya kisheria na kuwacha kufanya kazi kwa mazoea.
Nao madereva wa madaladala pamoja na madereva wa gari binafsi Omar Ali Wakizungumza na Zanzibar24 katika ziara ya ukaguzi wa magari yenye bima bandia wamesema wamelipokea zoezi hilo kwa masikitiko makubwa kutokana bado hawana uwelewa wa bima halali na bandia kwani bima zao wanakata katika shirika la bima zanzibar na kwenye matawi ya bima yaliyo karibu yao.
Zaidi ya Magari 100 yamekamatwa la mamlaka ya bima wakati wa ukaguzi wa bima bandia huko maruhubi.
chanzo:zanzibar24.
Comments