
Akijibu swali la msingi lililoulizwa na wawakilishi Jaku Hashim
Ayoub,Hidaya Ali Makame na Hassan Khamis Hafidh Naibu Waziri wa Wizara
hiyo Mmanga Mjengo Mjawiri amesema Serikali kwa kuliona tatizo hilo
imeanza kuchukua jitihada mbalimbali katika kuhakikisha wanaimarisha
mazingira ya watoto kujisomea, ili kuweza kupunguza idadi kubwa ya
wanafunzi katika madarasa ili kupata elimu katika mazingira bora kwa
maendeleo yao.
Amesema miongoni mwa jitihada hizo ni kuhamasisha jamii kupitia
kamati za skuli,kusaidia ujenzi wa madarasa ambapo jitihada za jamii
imeanza kuonekana ambapo jumla ya madarasa 285 yamejengwa katika ngazi
ya gebo na kukabidhiwa wizara kwa ajili ya kuyamaliza,jambo linaloitia
ari serikali kuyamaliza kwa haraka.
Hata hivyo amesema serikali imekuwa ikijenga mahusiano mazuri na
wahisani mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wakiwemo Zanzibar milele
Foundation ,Serikali ya watu wa China, Shirika la mswaada wa Sweeden,
ili kusaidia tatizo la madarasa linalowakabili kwa muda mrefu.
Aidha amesema katika mwaka 2017/2018 Wizara imetenga jumla ya fedha
billion 2,000,000,000 na bilioni 2 za wahisani, ili kusaidia
uwendelezaji wa miundombinu wa sekta ya elimu, ambapo fedha hizo
zitatumika kukamilisha jumla ya madarasa 200.
chanzo: zanzibar24.
Comments