Wazazi na walezi watakiwa kuwapeleka watoto wao katika vituo vya afya vilivyo karibu nao ili kupatiwa matone ya vitamen A, vidonge vya minyoo pamoja na kupima afya.

Image result for matone ya vitamen A, vidonge vya minyooMkuu wa kitengo cha lishe Pemba Nd.Raya Mkoko Hassan amewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kuanzia miezi 6 hadi miaka 5 katika vituo vya afya vilivyo  karibu nao ili kupatiwa matone ya vitamen A, vidonge vya minyoo pamoja na kupima afya zao ili kuwakinga na maradhi yanayoweza kuwakumba watoto katika umri huo.

Ameyasema hayo leo alipokua akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa jamuhuri hall uliopo Wete mkoa wa kaskazini ikiwa ni muendelezo wa mwezi wa lishe ya mtoto na kuwataka kushirikiana kwa pamoja kutoa elimu kwa jamii ili kuona zoezi hilo linafanikiwa kwa kiwango kinachohitajika.

Mkuu huyo amesema licha ya juhudi zinazochukuliwa na kitengo hicho ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano maeneo tofauti lakini bado wananchi hawajakuwa na muamko juu ya masuala hayo.

Mkoko amefahamisha kuwa  matone ya vitamen A humkinga mtoto na maradhi mbali mbali kama utapiamlo, kupofuka kwa macho  na maradhi mengineyo   ambayo ni hatarishi kwa afya yake.

Aidha amesema kuwa zoezi hilo hufanyika kwa mwaka mara mbili ikiwa ni kila baada ya miezi sita hivyo ni vyema wazazi kufikisha watoto wao bila ya kukosa.

Kwa upande wake Afisa wa kitengo cha lishe Pemba Nd. Massoud Omar Mohd  amesema wapo wanajamii wanaosema kuwa matone hayo yanakata uzazina kudai hilo sio kweli na kuwataka kuachana na dhana hiyo aliodai kuwa nipotofu.

Comments