Watu kadha wafariki baada ya moto kuteketeza jengo refu London.

Grenfell Tower Fire Watu kadha wamefariki baada ya moto mkubwa kuteketeza jengo refu usiku wa kuamkia leo mjini London.

Wazima moto bado wanakabiliana na moto huo katika jumba la Grenfell Tower, ambapo walioshudia walisema kuwa watu walikwama ndani, wakiitisha msaada.

Zaidi ya watu 50 wanatibiwa hospitalini.Moshi unaweza kuonekana kutoka mbali

Mwandishi wa BBC alisema kuwa kulikuwa na hofu kuwa jengo hilo lingeporomoka.

Moto huo katika jengo la Grenfell Tower ulianza mwendo wa saa 01:16, saa za Uingereza.Sehemu kubwa ya jengo ilishika moto
Idara ya wazima moto jijini London ilituma malori 40 ya kuzima moto huo.

 Mwandishi wa BBC Andy Moore aliyepo katika eneo la tukio alisema jengo hilo liikubwa na wasiwasi wa kuanguka.
chanzo:Bbc. Grenfell Tower Fire

Comments