Wakulima wa Mpunga Bonde la Mjumbe Kangagani Pemba watarajio mazuri ya mavuno kulinganisha na misimu iliopita.

Image result for mabonde ya mpungaLICHA ya mvua kubwa zilizonyesha na kuathiri maeneo mengi ya makaazi pamoja na maeneo ya kilimo, Wakulima wa Mpunga Bonde la Mjumbe Kangagani wameeleza furaha yao ya wanamatarajio mazuri ya mavuno kulinganisha na misimu iliopita.

Wakitoa maelezo juu ya kufurahishwa kwao kutokana na kupata mbegu bora za kisasa huko Kangagani, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.


Wakulimahao, wamesema kwa sasa hawahitaji kurudi nyuma katika masuala ya kilimo walichozoea na kurithi kwa wazee wao, bali wataendelea na ukulima wa muda mfupi ambao utawaondolea kero ya kujikimu kwa chakula kwa wakati.

Mmoja kati ya wakulima wa Mpunga katika bonde hilo, Time Bakar Hassan, amesema kuwa wamepata tofauti kubwa ya uotaji na uzalishaji wa mpunga baada ya kupatiwa mbegu za muda mfupi na kufuata maelekezo ya wataalamu.

Sambamba na hayo, Mwahaji Suleiman Haji, amesema kuwa, wataalamu wa masuala ya kilimo imefikia pahala stahiki kupewa pongezi kwa kuwasaidia kwa karibu mbinu bora za uzalishaji ambazo zitachangia katika kuwakwamua na ukali wa maisha.

Kwa upande wake, Khamis Zuber Kassim, amewashauri wakulima wenzake kufuata maelekezo wanayopatiwa na wataalamu wa masuala ya kilimo, ili waweze kupata mabadiliko ya haraka yenye tija kwa faida yao.

Hata Hivyo ameiomba Idara husika kuendelea kutoa taaluma inayokwenda na wakati, kila muda unaporuhusu, ili kuwasaidia kupata mavuno mazuri.

Nae Afisa Mkuu Idara ya Umwagiliji Maji, Mbarouk Ali Mgau, Amesema kuwa tofauti ya mapato ya mavuno yatakuwa mazuri kulinganisha na wakati uliopita kwa wakulima waliokubali mabadiliko .

Aidha amewataka wakulima kufuta ushauri na mbinu wanazopatiwa na wataalamu kulinganisha na hali ya hewa wanaweza kukomboka kiuchumi kwa kupata mafanikio zaidi.

Comments