Ving’amuzi viwili vyamsotesha rumande.

mahakama ya mwanzo Chwaka imemtupa rumnde wiki mbili mtuhumiwa Hassan Othman Ali (32) mkaazi wa Ndijani skuli kwa kosa la kuiba ving’amuzi viwili mali ya mali ya Hassan Haji Ameir.

Mtuhumiwa huyo alijiripua mahakamani hapo kwa kukubali kosa lake la kuiba ving’amuzi hivyo kimoja cha Azam TV na kingine cha Star Times vikiwa nathamani ya shilingi lakimbili kwa kukisia.


Upelelezi1 wa shauri hilo umeshakamilika na mtuhumiwa amepelekwa rumande hadi tarehe 16/6 mwaka huu shauri lake litakapo sikilizwa tena na kutolewa hukumu.
chanzo:zanzibar24.

Comments