Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana liliidhinisha suala la kutumwa wanajeshi zaidi katika eneo la Sahel huko Afrika kwa shabaha ya kupambana na makundi ya waasi.
Azimio lililopasishwa na Baraza la Usalama limesema kuwa, nchi wanachama wa kundi la G5 Sahel ambazo ni Mali, Mauritania, Niger, Chad na Burkina Faso zinapaswa kutuma wanajeshi elfu tano zaidi katika eneo hilo.
Kikosi cha nchi hizo tano chenye askari elfu kumi kinaongozwa na Didier Dacko kutoka Mali.
Eneo la Sahel Afrika lenye jamii ya watu karibu milioni mia moja ni miongoni mwa maeneo nyeti na yenye migogoro ya mara kwa mara barani Afrika. Eneo hilo linakabiliwa na vitisho vya makundi kama Boko Haram, Al Qaida, Daesh na waasi. Mgogoro wa ndani nchini Libya pia umechochea zaidi hali ya ukosefu wa amani katika eneo hilo.
chanzo:parstoday.
Comments