
Mamlaka hiyo imesema, kwa muda mrefu wamiliki wa vyombo vya moto,
wamekuwa wakiuziwa bima zisizostahiki bila ya wao kujua, ingawa kwa sasa
kwa wauzaji hao, mwisho wao umefika.
Akizungumza kwenye mafunzo ya siku moja, yaliowahusishwa askari wa
kikosi cha usalama barabarani na kufanyika skuli ya sekondari Madungu
Chakechake, Mkurugenzi wa Masoko na utafiti wa Mamlaka hiyo Adelaida
Muganyizi alisema sasa bima zote zitahakikiwa kwa njia ya kielektroniki.
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa, kwa vile kisheria kila kampuni au
wakala wa kuuza bima anatakiwa awe amesjaliwa na Mamlaka ya usimamizi wa
bima Tanzania ‘TIRA’ itakuwa ni rahisi kuwashika wale mawakala
wanaofanyakazi zao kimagumashi.
Alieleza kuwa, kupitia mfumo wa kisasa wa kuandika neno stika
ikifuatiwa na namba ya bima na kuituma kwenda namba 15200, kwa milikiwa
gari au chombo cha moto atagundua uhalali wa wakala huyo.
“TIRA baada ya kukaa na wataalamu sasa imekuja na mfumo wa kidigitali
kwa anaenunua bima kabla ya kulipa, atafuata maelekezo hayo na kutuma
kwenye namba husika, na hapo sasa atagundua kuwa muuza bima huyo
anatambuliwa na ‘TIRA’ au ni wa mitaani”,alieleza.
Kwa upande wake Menaja wa ‘TEHAMA’ wa Mamlaka hiyo Aron Malaki
alisema, kazi iliopo mbele yao kwa sasa, ni kutoa elimu kwa wamiliki wa
vyombo vya moto na wananchi wengine, juu ya kufuata mfumo huo wa kisasa.
“Faida yake hasa kwa abiria, iwapo gari haina bila halali ni vigumu
unapopata ajali au kukugongwa kupata fidia kutokana na mauimivu
ulioyapata kwa vile uhalali wa bima haupo”,alifafanua.
Mapema baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wa siku moja, wameiomba
‘TIRA’ kuhakikisha elimu hiyo wanaisambaaza kwa jamii nzima, ili
kuhakikisha inawafikia.
Hata hivyo walisema kwa sasa wataondokana na ile njia ya zamani ya
kukagua bima kwa kuangalia rangi na tarehe iliokatwa au kumalizika, na
sasa kwa kutumia mfumo wa kisasa watafanyakazi wa uweledi.
chanzo: zanzibar24.
Comments