
malalamiko hayo yamebainishwa na katibu wa kudumu wa wizara ya
biashara na uwekezaji Profesa Adolf Mkenda kuwa serikali ya tanzania
imegundua katazo hilo kupitia vyombo vya habari mjini Nairobi kwamba
Kenya imepiga marufuku uingizwaji wa gesi ya kupika kutoka Tanzania
kupitia mpaka wa Kenya na Tanzania.
Amesema kufanya hivyo ni kinyume na makubaliano ya jamii ya Afrika
mashariki na makubaliano waliyoafikiana baina ya Kenya na Tanzania
baada ya Kenya kuiwekea marufuku Tanzania mnamo mwezi Mei 18, 2017.
Aidha Profesa Mkenda amesema hatua hiyo ya Kenya itaathiri
wafanyibiashara na raia wa kawaida wanaoendesha maisha yao kupitia
biashara ya kuuza gesi .
Amesema katika mkutano wa Jamii ya Afrika mashariki ulio fanyika
mwezi juni 2- 2017 ulio wakutanisha pamoja mawaziri wa biashara na
viwanda iliamuliwa kwamba Kenya ilifaa kuondoa marufuku ili kuafikia
makubaliano hayo ya Afrika mashariki.
kwa wakati huo Kenya ilikubali kuondoa marufuku hiyo ya ununuzi wa gesi kutoka Tanzania kupitia mpaka wa mataifa hayo mawili.
Hivyo Profesa Mkenda amesema kuwa serikali ya Tanzania itaendelea na mpango wa kutatua tatizo hilo.
Kwa upande wake katibu maalum nchini Kenya Andrew Kamau amesema
kupitia gazeti la The Citizen nchini Tanzania, Siku ya Jumatatu
limeandika amesema kuwa wafanyibiashara hawataruhusiwa kununua gesi
kupitia mipakani katika kipindi cha juma moja.
Amesema hatua hiyo inalenga kuzuia kampuni haramu zinazouza gesi ambazo zimeathiri usalama wa taifa hilo.
Chanzo:zanzibar24.
Comments