
Akizungumza na mwanahabari wetu juu ya hatua za kuchukuwa wakulima
ili zao hilo liweze kuwanufaisha wananchi katika kipindi cha mvua na
kiangazi mtafifi wa sayansi ya bahari Dk.Flower Ezekiel Msuya amesema
wakulima wanashindwa kuendelea na kilimo kutokana na mwani kuharibika na
kupelekea kukosa mbegu za kuendelea na kilimo hicho.
Amesema pindipo serikali itachukuwa jukumu la kuhifadhi mbegu hizo
zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuwawezesha wakulima kuzalisha mwani
unaolingana na mahitaji ya soko na kuweza kuleta maendeleo ya haraka
katika Nchi.
Kwa upande wake Afisa Mupango kutoka shirika la Maendeleo ya Viwanda
ya Umoja wa taifa kutoka (UNIDO) Gerald Runyoro wa amesema
watashirikikana na serikali katika kutafutia masoko ya zao hilo ili
wakulima waweze kunufaika na bei nzuri zinazotokana na bidhaa
wanzozalisha pamoja na kutowa wito kwa watafiti hao , kuwa na utaratibu
wa kufanya utafiti katika mazao ya baharini ili wakulima waweze
kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.
Akifunga mkutano huo wa siku mbili Naibu katibu mkuu wa wizara ya
kilimo ,Dk.Islam Seif amewataka wakulima wa mwani kufuata taratibu za
kiafya walizopangiwa ili waweze kulima mwani wenye ubora wakati
serikali ikiendelea na kufanya tathmini juu ya kuyapatia ufumbuzi wa
muda mrefu maradhi yalivamia zao la mwani.
chanzo:Zanzibar24.
Comments