SMZ: Viongozi watakao danganya fomu za maadili kuchukuliwa hatua.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe. Haroun Ali Suleiman amesema atahakikisha na kusimamia kwa umakini kuhakikisha kila kiongozi amechukua fomu za maadili na kuorodhesha mali zao ili kuepuka udanganyifu kwa viongozi wa serikali.

Aidha Waziri Haroun aliongeza kuwa endapo kiongozi ataepuka kujaza au kufanya udanganyifu wowote katika fomu hiyo atachukuliwa hatua za kisheria, huku tayari jumla ya fomu 1600 zimepokelewa.


Akizungumzia kuhusiana na Rushwa pamoja na uhujumu wa uchumi, Waziri Haroun amesema katika kesi za rushwa na uhujumu wa uchumi Zanzibar kwa makosa mbalimbali yakiwemo yakupokea rushwa, matumizi mabaya ya ofisi na mali za umma  pamoja na kukwepa kulipa kodi mamlaka imefanya udhibiti na kugundua  makosa 71 ambapo majalada 11 yapo kwa DDP na 4 yapo mahakamani.

chanzo:Zanzibar24

Comments