Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekusudia kuanzishwa wakala wa Ulinzi watakaoshirikiana na askari wa vikosi vya usalama kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi hususan katika ukanda wa bahari.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Baraza la wawakilishi la zamani Kikwajuni,Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa,
Serikali za mitaa na idara maalum za SMZ, Haji Omar Kheir amesema uwepo wa uwakala huo utaimarisha ulinzi pamoja na kupambana na vitendo viovu vinavyofanywa na baadhi ya watu katika jamii.
Aidha amesema hatua hiyo pia itavipunguzia majukumu Vikosi vya idara maalumu kulinda taasisi za kiserekali na maeneo ya wawekezaji, na kuvifanya viweze kutekeleza majumu yao ya kulinda ulinzi na usalama wa nchi.
Amesema katika kutekeleza azma hiyo serikali itaajiri vijana wa Jeshi la Kujenga uchumi JKU ambao wamepewa mafunzo ya ulinzi ikiwemo kuweza kutumia dhana wanazotumia askari wengine ili kuwa wakala wa ulinzi ambao watatambulika kisheria katika utekelezaji wa majukumu yao kwa wananchi.
chanzo: Zanzibar24.
Comments