
Matumaini ya kumalizika kwa kero hiyo yamekuja kufuatia Mwakilishi wa
jimbo la Tunguu Simai Mohammed Said kukabidhi mipira sita ya kusambazia
maji iliyogharimu shilingi 2,500,000.
Kwa miaka mingi, wananchi wa eneo hilo lenye historia kubwa kwa kuwa
ndiko alikozaliwa Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Abeid Amani
Karume, wamekuwa wakitumia maji ya visima ambayo hayana uhakika wa
usalama.
Akizungumza kwa niaba yake na Mbunge wa jimbo hilo Khalifa Salum
Suleiman wakati wa makabidhiano hayo, Mwakilishi Simai alisema msaada
huo ni miongoni mwa malengo yao ya kuwaondoshea wananchi shida
mbalimbali zinazowakabili hatua kwa hatua.
Alisema baada ya kupokea taarifa kutoka uongozi wa wadi ya Ubago juu
ya tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama, na sasa wanaanza
harakati za kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi.
Alifahamisha kuwa baada ya kutandikwa mipira hiyo ikiwa awamu ya
kwanza, juhudi zitaendelea kufikisha maji kutoka Kwa kozi hadi Mkorogo,
ili kuhakikisha viambo vyote vinapata maji kutoka masafa ya karibu.
Hata hivyo, aliwakumbusha wananchi wahakikishe kuwa mipira hiyo
hawaitandiki karibu na hifadhi ya barabara, akisema iko katika mipango
ya serikali kuitengeneza, kwani nayo ni miongoni mwa kero za muda mrefu
zinazowakabili wanakijiji wa huko.
“Mbali na hapa, pia tuko katika juhudi za kuhakikisha maeneo yote ya
jimbo letu la Tunguu yanaondokana na shida ya maji, hivyo tunaiomba
Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) ituunge mkono,” alisema Simai.
Alitoa wito kwa vijana wa eneo hilo kujitokeza kwa wingi wakati wa
kuchimba msingi utakaotandikwa mipira hiyo ili hatimaye maji yaweze
kupatikana kirahisi.
Naye Diwani wa wadi ya Ubago Ussi Ali Mtumwa, alisema baada ya kupata
mipira hiyo, sasa ni kazi tu, na kutaka wananchi wapange siku ya kuanza
shughuli na kuimaliza haraka ili kutoa nafasi ya kuendelea na hatua
nyengine.
Alisema mbali na changamoto ya maji, pia wanahitaji kujengewa
barabara kwa kiwango cha lami, kwani kwa sasa iko katika hali mbaya.
chano: zanzibar24.
Comments