Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angella
Kairuki alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza
la Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi (Chadema).
Mkundi alitaka kujua ni
lini serikali itawalipa stahiki zao walimu wa Hesabu, Sayansi na
watalaamu wa maabara waliopangiwa vituo hivi karibuni. Alisema
halmashauri zote zilizopokea walimu hao zinapaswa kuwapa posho za
kujikimu ndani ya siku saba.
Akijibu swali la msingi la Mkundi aliyetaka kujua serikali ina mpango
gani wa kutoa posho za mazingira magumu kwa watumishi wa maeneo ya
pembezoni, alisema, “Katika kutekeleza Sera ya Malipo ya Mishahara na
Motisha iliyopitishwa mwaka 2010, mwaka 2012/13 halmashauri 33 za wilaya
ikiwemo halmashauri ya Ukerewe ziliwezeshwa kuandaa miongozo ya kutoa
motosha kwa watumishi.”
Alisema kutokana na mpango huo, halmashauri 29 ziliandaa na
kuwasilisha katika ofisi ya wizara hiyo miongozo iliyobainisha aina ya
motisha inayohitajika. “Utekelezaji wa miongozo hiyo kwa halmashauri
zote 29 ulikadiriwa kugharimu Sh bilioni 331.087 kwa mwaka na
utekelezaji wa miongozo hiyo, ulitarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha
wa 2013/14 na haukuanza kutokana na ufinyu wa bajeti.
chanzo:Habarileo.
Comments