
Nyumba hiyo yenye vyumba tisa inapatikana katika mtaa wa kifahari wa Kalorama na iliuzwa $8.1m (£6.2m).
Obama
ameamua kuendelea kukaa Washington na familia yake hadi binti yake
mdogo, Sasha ambaye ana umri wa miaka 15, amalize masomo ya shule ya
upili.
Kiongozi huyo na mkewe Michelle wamekuwa wakizuru mataifa mbalimbali duniani tangu walipoondoka White House mwezi Januari.
Msemaji
wa Bw Obama, Kevin Lewis, alithibitisha ununuzi huo na kusema:
"Ikizingatiwa kwamba Rais na Bi Obama watakuwa Washington kwa angalau
miaka mingine miwili unusu, ina umuhimu kwao kununua nyumba badala ya
kuendelea kukodi."
Kuna vizuizi vya saruji kuzuia watu kufikia
nyumba hiyo yenye ukubwa wa futi mraba 8,300 (mita mraba 770), ambayo
inalindwa saa 24 kila siku na maafisa wa kikosi cha kulinda marais
Marekani.
Familia ya Obama bado inamiliki nyumba Chicago.
Walinunua nyumba hiyo kutoka kwa aliyekuwa afisa wa habari wa Bill Clinton Joe Lockhart, aliyeinunua mwaka 2014 kwa $5.3m.
Nyumba
hiyo haiko mbali sana na nyumba ya thamani ya $23m inayomilikiwa na
mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos, ambaye pia humiliki gazeti la
Washington Post.
Bintiye Rais Donald Trump, Ivanka, na mumewe
Jared Kushner ambaye kwa sasa ni mshauri mkuu White House, pia wanaishi
hapo karibu.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson ni
afisa mwingine wa ngazi ya juu anayeishi Kalorama, katika nyumba
aliyoinunua kwa $5.6m Februari.
chanzo:Bbc.
Comments