Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbulu
Vijijini, Flatei Massay (CCM) aliyetaka kujua ni lini serikali itaziba
mapengo ya watumishi hasa wa afya walioondolewa kutokana na sakata la
kuwa na vyeti feki.
Majaliwa alisema ni kweli uhakiki umefanyika na
serikali ikabaini kwamba baadhi ya wafanyakazi walikuwa na vyeti feki.
Alisema wengine walikuwa na vyeti ambavyo ama vinatumika mara mbili kwa
watu zaidi ya mmoja.
“Lakini wapo waliobainika kwamba kuna utata katika majina katika
vyeti hivyo, ambao ndio waliruhusiwa kukata rufaa na leo ndio siku ya
mwisho ya kuangalia tatizo hilo,” alisema.
Alisema baada ya uhakiki
kukamilika, Rais John Magufuli tayari ameshatoa vibali vya kuajiri zaidi
ya watumishi 50,000 na anaendelea kutoa na kinachoangaliwa zaidi ni
kuziba mapengo ya watalaamu kwenye sekta mbalimbali.
chanzo:Habarileo.
Comments