Mganga Mkuu wa Mkoa, Leonard Subi akizungumza kwenye mahojiano na Mwananchi leo anasema kuwa mkoa unatumia chupa 30,000 kwa mwaka.
Amesema kwamba, mtu akitoa damu anakuwa amejiweka katika nafasi nzuri hususan anapokuwa amepata tatizo la uhitaji kwani mwanzoni anapochangia hupewa kadi maalum.
Hata hivyo, mkoa umekuwa ukikusanya chupa 45 kwa siku, badala ya chupa 80 za damu salama na hivyo kuwa katika uhitaji au uhaba wa chupa 35.
"Bado hatukidhi mahitaji ya damu kwa kweli, hii inamaanisha wananchi wengi hawataki kujitolea katika kuchangia damu," anasema Subi.
Kwa upande wake,ofisa uhamasishaji wa damu salama Kanda ya Ziwa, Bernadicto Medaa, amesema kutokana na uhaba wa damu salama, walizindua kampeni ya uchangiaji damu tangu Juni 2 mwaka huu, na wanatarajia kupata chupa 4000 hii leo.
Comments