Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu la kieneo ameashiria matatizo mengi na mahitaji chungu nzima ya wakimbizi wa Syria na kueleza kuwa, mahitaji ya wakimbizi hao yapo nje ya uwezo wa mashirika hayo ya kimataifa.
Magne Barth amesema kuwa, operesheni za kibinadamu za Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu huko nchini Syria ndio operesheni kubwa kabisa iliyowahi kufanywa na shirika hilo duniani.
Afisa huyo wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu amesema kuwa, takribani nusu ya raia wa Syria ni wakimbizi na kuongeza kuwa, shirika hilo lina uwezo kwa sasa wa kudhamini mahitaji ya haraka na ya dharura ya kibinadamu kwa wakimbizi hao.
Baadhi ya ripoti za Umoja wa Mataifa na mashirika ya utoaji misaada ya kibinadamu zimekuwa zikitahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea maafa ya kibinadamu nchini Syria kutokana na hali mbaya inayowakabili wakimbizi wa nchi hiyo.
Syria ilitumbukia katika mgogoro wa kutwishwa mwaka 2011 baada ya makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Saudi Arabia, Marekani na waitifaki wake ikiwemo Uturuki, kuanzisha mashambulio makubwa ya kijeshi kwa ajili ya kuiondoa madarakani serikali halali ya Rais Bashar al-Assad.
chanzo:parstoday.
Comments