Mrithi wa Prof. Muhongo awasilisha bajeti ya wizara Bungeni.

Kufuatia kutokuwepo kwa Waziri wa Nishati na Madini Bungeni, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ameteuliwa kuwasilisha makadirio ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwa wa fedha 2017/18.
Waziri Mwijage ameteuliwa kuwasilisha bajeti hiyo leo bungeni baada ya Rais Dkt Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo Mei 24 mwaka huu ikiwa ni wiki moja kabla ya bajeti kuwasilishwa.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
Katika bajeti hiyo inayowasilishwa leo, majadala katika sekta ya madini ndio unatarajiwa kuchukua nafasi kubwa kutokana na ripoti ya Prof. Mruma iliyowasilishwa kwa Rais kuhusu makinikia yaliyozuiwa bandarini.
chanzo:zanzibar24.

Comments