
Akisoma hutuba ya mswada wa sheria ya ushuru wa Bidhaa Dk.khalid
amesema mswada huo utaimarisha mazingira ya uwekezaji Nchini kwa kuondoa
utata juu ya mamlaka ya usimamizi ,utoaji na ukusanyaji wa ushuru.
Amesema mswada huo pia utalinda na kuongeza mapato ya serikali
yanayotokana na vyanzio husika pamoja na kuwa na msingi thabit wa
kisheria wa usimamizi wa ushuru huo na kuwepo ushuru wa kulinda hali ya
kijamii na uhumi wa Zanzibar.
Akizungumzia Mswada wa sheria ya ushuru wa Stempu itakayochukuwa
Nafasi ya sheria wa ushuru wa stempu NAM 6 ya Mwaka 1996 Waziri Khalid
amesema mswada huo umegawika katika sehemu tano utaoweza kutoa fursa kwa
wafanya biashara wadogo kulipia kodi kwenye taasisi moja ya ZRB.
Hata hivyo amesema mswada huo pia utaeka utaratibu bora na viwango
maalumu vya kodi kwa wafanya biashara wadogo wa bidhaa na huduma na
usimamizi wa ukusanyaji kodi kwa wafanya biashara waliokuwa
hawakusajiliwa kwa viwango vya VAT.
Kwa kipindi kirefu wafanya biashara Wadogo walikuwa wakilalamikia
gharama za ulipaji kwa kutakiwa kilipia kodi katika taasisi mbili na
ukubwa wa kodi ambapo mswada huo utawasaidia kutatua matatizo
yanayowakabili.
chanzo;Zanzibar24.
Comments