Malinyi tumieni kwanza Simbanking.

Serikali imewataka wananchi wilayani Malinyi mkoani hapa kuendelea kutumia huduma za kifedha zinazotolewa na kampuni za simu za mkononi mpaka mkakati wa kuanzishwa kwa tawi la benki utakapokamilika.
Msimamo huo umetolewa leo (Ijumaa) bungeni na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Malinyi, Dk Hadji Mponda aliyetaka kujua ni lini wilayani hiyo itapata huduma za benki.
"Wananchi wa Malinyi wanashauriwa kutumia njia mbadala kupata huduma za kibenki ikiwamo kupitia simu za mkononi yaani simbanking ya CRDB na banking on the wheel ya NMB iliyopo Mlimba kwa kipindi hiki," amesema Dk Kijaji.
Waziri huyo amefafanua kwamba Malinyi ni moja ya wilaya zinazonufaika na huduma za mawakala wa Fahari Huduma zinazoendeshwa na Benki ya CRDB kufungua akaunti, kuweka na kuchukua fedha, kuomba mikopo na kupata ushauri wa huduma za fedha.
chanzo:Mwananchi.

Comments