Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeitaka serikali kurasimisha maeneo mapya ya utalii na kuboresha yaliyopo ili kukuza utalii wa ndani na wa kimataifa.
Pia LHRC, kimeishauri serikali kuendeleza mchakato wa upatikanaji wa katiba ya wananchi ambayo italeta mabadiliko ya sheria katika sekta ya maliasili, madini na ardhi ili kila mtanzania aweze kunufaika na rasilimali za nchi.
Hayo yameelezwa jana na Ofisa Programu wa LHRC, Pasience Mloe kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, wakati wa ziara ya wafanyakazi wa kituo hicho kwenye mbuga ya hifadhi ya Saadan ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani.
"Kituo kinatoa pongezi kwa serikali kwa kuona umuhimu wa kuhamasisha utalii wa ndani na kutoa vibali kwa wananchi kutembelea hifadhi za mbuga mbalimbali kwa siku tatu bila malipo," amesema Mloe.
Amesema kuna vivutio vingi vya utalii vyenye uwezo wa kuongeza mapato kwenye sekta hiyo, lakini havijarasimishwa hivyo ni mda muafaka kwa serikali kufanyia kazi eneo hilo.
Comments