Kuku mweusi amsababishia kutupwa rumande kwa muda wa wiki mbili.

Mahakama ya mwanzo Mfenesini imempandisha kizimbani mtuhumiwa Saidi Ali Omar (24) mkaazi wa Mahonda Mto Mchanga kwa kupatikana na kosa kuiba kuku mwenye rangi nyesi pamoja na mayai yake.

Mnamo tarehe 27 Disemba mwaka jana mtuhumiwa huyo alimuiba kuku huyo na mayai yake mwenye thamani ya shilingi elfu tano kwa kukisia  mali ya Ali Omar Khamis mkaazi wa Mahonda mto mchanga.


Baada ya kusomewa kosa lake mtuhumiwa huyo alikataa na kuiomba mahakama impe dhamana ombi ambalo mlilikataliwa na kuamuriwa kwenda rumande kwa muda wa wiki mbili hadi kesi itakapotajwa tena.
chanzo: zanzibar24.

Comments