
Akijibu swali la msingi lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Paje
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara
maalumu za SMZ Haji Omar Kheri amesema utaratibu wa kuwapata tena
wanyama hao kwa wamiliki wa mifugo hiyo ni kuchukua barua katika
Shehia anayofugwa mnyama husika na kuiwasilisha barua hiyo ya utambuzi
katika Manispaa yao.
Hata hivyo Haji amesema lazima mfugaji alipie gharama za utunzaji wa
wanyama hao kwa kipindi chote alichokaa mnyama katika hifadhi ya
serikali na atakabidhiwa mnyama wake akiwa amewekwa alama maalum kwa
lengo la udhitibi wa kurudi tena kuwaweka wanyama hao katika maeneo
yasiyoruhusiwa kufuga.
Aidha amefafanua kuwa endapo mnyama huyo aliyeekewa alama
atakamatwa tena katika maeneo yasiyoruhusiwa mnyama huyo atakuwa mali ya
Serikali na taratibu husika za kuuzwa zitafuatwa.
chanzo: zanzibar24.
Comments