
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Bi.Nagma Giga
wakati akikabidhi vitendea kazi ambavyo ni komputa na priter kwa Mikoa
na Wilaya nane za jumuiya hiyo huko katika Afisi Kuu ya Wazazi Mpirani
Kikwajuni Unguja.
Alisema
watendaji wa ngazi za mikoa na wilaya za jumuiya hiyo ndio wasimamizi
wakuu wa uchaguzi huo kwa ngazi mbali mbali za jumuiya hivyo wakati wa
kuchuja wagombea ni lazima waweke kando urafiki na undugu na wawapitishe
viongozi wenye sifa na uzalendo wa kukisaidia chama kushinda katika
uchaguzi mkuu ujao.
“Mafanikio
tuliyonayo ndani ya jumuiya yrtu yanatokana na juhudi zenu za
kiutendaji hivyo nakupongezeni sana na muendelee na kasi hiyo hiyo hadi
tupate viongozi imara watakaotetea maslahi ya CCM mwaka 2020”,.alisema
Giga.
Aidha
aliwasisitiza viongozi hao kuhakikisha wanatunza vizuri vifaa
walivyopewa na kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili kurahisisha
shughuli za kiutendaji za jumuiya.
chanzo:zanzibar24.
Comments