Jeshi la polisi mkoa wa kusini Pemba lasema kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya Laurent Intanational School iliyopo Ole Kianga hakikutokana na kupigwa na mwalimu kama inavyodaiwa.

Akizungumza na
wandishi wa habari huko ofisini kwake Madungu Chake Chake Pemba amesema
kuwa mnamo tarehe 30/05/2017 majira ya
saa 5;00 asubuhi walipokea taarifa ya
kifo cha mwanafunzi huyo na ndipo wakachukua hatua za haraka kufika shuleni
hapo kuhoji walimu pamoja na wanafunzi wa shule hiyo na katika
taarifa za awali uchanguzi huo ulibaini kwambo mwanafunzi huyo alipata adhabu
baada ya kuharibu midoli ya kufundishia wanafunzi wa chekechea shuleni hapo.
Shekhan
amesema,kabla ya hapo awali alipata kuanguka
chooni na kuumia sehemu ya bega la mkono wa kulia na alianza kupatiwa
matibabu ya awalii na daktari wa shule hata hivyo hali haikua nzuri na
kulazimika kupelekwa hospitali ya Chake Chake na Mwanamashungi kwa matibabu
zaidi.
Amefahamisha
kuwa 25/05/2017 baba wa mtoto huyo alifika shulenio hapo kwa ajili ya kumchukua
na kwenda nae nyumbani kwa lengo la kumpeleka hospitali ya Wete kwa matibabu
zaidi aliruhusiwa kurudi nae nyumbani na ilipofika 29/05/2017 alirejeshwa tena
hspitali ya wete na kulazwa na hatimae majira ya saa08;00 alifariki dunia.
Aidha amesema
kwa sasa wanawashikilia watu saba na uchunguzi ukikamilika watapandishwa
mahakamani kwa kujibu shtaka la uzalilishaji pomoja na uzembe na sio shtaka la
mauaji.
Comments